Ijumaa , 22nd Sep , 2017

Msanii Madee ambaye ni meneja wa msanii Dogo Janja, amejibu tuhuma zilizotolewa na wasanii wa Uganda Weasel & Radio, kwamba hawajui collabo yao na Dogo Janja iliishia wapi, kwani baada ya kuifanya hakukuwa na mwasiliano yoyote.

Akizungumza na mwandishi wa habari wa East Africa Television, Madee amesema baada ya kuachia wimbo huo huku wakitarajia kufanya video yake, wasanii hao walikuwa wakimwambia wako busy sana, hivyo wakashindwa kufanya video hiyo mpaka sasa.

Madee aliendelea kusema kamba pamoja na hayo pia promo ambayo ilifanyika ilikuwa ni hapa hapa bongo, kutokana na kwamba wenzao walikuwa na ratiba za kubana sana hivyo haikuweza kufika kwa kiasi kubwa nchini Uganda, na kwengineko Afrika Mashariki.

Weasel & Radio walihojiwa kwenye kipindi cha The Cruise cha East Africa Radio wiki hii, na kusema hawajui collabo yao hiyo iliishia wapi, huku wakidai kuvunjika kwa mawasiliano kati yao na Dogo Janja.

Msikilize hapa chini