Jumatano , 28th Jun , 2017

Rapa Lordeyes Mweusi wa N2N, amedai toka alipoamua rasmi kurudi kwenye game ya muziki wa hip hop atakuwa anaachia mikwaju mfululizo ili kuwapa tiba mashabiki wake ambao walikosa muziki mzuri kutokana na  kukosekana kwa mrithi wa nafasi yake.

Rapa Lordeyes

Leo wakati akitambulisha ngoma yake mpya  kwa mara ya kwanza ndani ya Planet Bongo ya East Africa Radio 'Manyota wa Mtaa', Lordeyes amesema kwamba anatambua ni jinsi gani mashabiki wanaugua kwa kukosa muziki mzuri kwani hakuna mtu aliyeweza kuziba pengo lake hata baada ya kukaa muda mrefu nje ya game.

"Najua watu wangu walikosa ile ladha ya  'African hip hop' ambayo tunayo wachache sana. Kiti changu ni kama cha Albert Mangwea yaani tangu alipoondoka wamepita kujaribu kuziba pengo lake na imeshindikana,  Sasa kwa upande wangu nmerudi kwenye kiti maana watu walishindwa kutumia fursa wakati nipo nje ya game sasa nimerudi mwenyewe. Mashabiki zangu najua jinsi ya kuponya ugonjwa wao yaani kazi juu ya kazi tutaenda sawa tu, najua tiba yao.

Aidha Lordeyes amewasihi mashabiki zake wasikate tamaa kwani ladha za hip hop za Afrika wanazozisikia kutoka kwa wasanii wa kimataifa kama Sarkodie na wengine watazisikia mfululizo kutoka kwake.

Loreyes ameachia ngoma aliyomshirikisha mnako mwenzake G Nako huku Bugalee akiwa ndiyo mpishi wa wimbo huo uliopewa jina la Manyota wa Mtaa.