Linex azidi kulia na wapenda kiki

Monday , 20th Mar , 2017

Msanii Sunday Mjeda (Linex) amewashauri wasanii wenzake kuacha kutegemea skendo (kiki) katika kufanya kazi zao wanazotarajia kuzitoa kwa jamii.

Linex

Linex amesema kitendo hicho kinapelekea kudidimiza soko la muziki na filamu kwa sababu vipaji vingi vinapotezwa huku wasiokuwa na vipaji ndiyo wakiendelea ku-hit katika soko la biashara la sanaa.

“Nachoweza kusema turudi kushabikia muziki mzuri, tuache kushabikia skendo, nachokiona hapa muziki unapotea kabisa”. Alisema Linex

Aidha msanii huyo amesema endapo wasanii wenzake hawatataka kubadilika kutoka katika hilo jambo basi muziki mzuri utabakia kuwa historia katika masikio yetu huku akiwataka mashabiki kurudi katika ushabiki wa muziki mzuri sio kushabikia skendo za watu maarufu.