Ijumaa , 5th Mar , 2021

Msanii wa BongoFleva Juma Jux amesema anapenda sana nyumba nzuri hivyo hata ule mjengo wake mpya anao-post Instagram anaona bado hajafikia nyumba ambayo anataka iwe ya ndoto zake.

Picha ya Jux na mjengo wake mpya

Jux amesema mjengo wake wa sasa upo vizuri lakini bado anajaribu kujenga nyumba nyingine zaidi ya hiyo 

"Ile bado sio nyumba ya ndoto yangu na ambayo nataka kuishi japo tunajaribu tu kidogo na Mungu katujaalia, pale nakaa ndiyo lakini sio nyumba ya ndoto yangu mimi napenda sana nyumba na vitu vizuri, bado naendelea kupambana ili kufikia nyumba ambayo nataka niwe nayo" amesema Jux 

Mtazame hapa Jux akizungumzia hilo.