Jumanne , 27th Oct , 2020

Msanii Zee Cuty amemuomba msamaha Shilole kufuatia picha na video zinazo-trend mitandaoni zikimuonyesha akikumbatiana na aliyekuwa mume wake Uchebe kwa kusema jambo hilo hakufanya kwa kiki wala kusudio lake sio kumuumiza.

Msanii Zee Cuty upande wa kushoto, kulia ni Uchebe na Shilole

Akizungumzia tukio hilo Zee Cuty mwenyewe amesema kuwa  "Mimi na Uchebe tunafahamiana kwenye mazingira ya kazi na alikuwa mume wa dada yangu Shilole ila kuna watu wanadhani nimeingia kwenye kiki na Uchebe, namuheshimu kama mtu ambaye alikuwa na dada yangu, kilichotokea ni salamu tu na nilikuwa nipo kwenye hali ya ujana fulani hivi

"Nilikuwa namsalimia kawaida sio kama nimemkumbatia vibaya, sikuwaza kama watu watafikiria hivyo na kwa comments zao zimeni-disappoint sana, na sikuwahi kutegemea kama nitakuja kumkwaza dada Shishi kama nimemkosea au amechukia namuomba msamaha, nahisi amejisikia vibaya" ameongeza 

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.