Jumatano , 11th Jan , 2017

Msanii Angel-Mary Kato ambaye amewahi kushiriki mashindano ya BSS mwaka 2015 na kuibuka mshindi namba nne katika mashindano hayo amefunguka na kueleza kilichomo kwenye ngoma yake mpya ya 'No Stress'

Angel-Mary

Amesema kuwa wimbo huo ni wimbo ambao unagusa maisha yake moja kwa moja kwani wimbo huo aliandika siku ya tatu baada ya kuachwa na mpenzi wake.

Angel Mary akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo amesema kwake yeye ilikuwa ni mara ya kwanza kuumizwa na mapenzi, kwani aliachwa na mtu ambaye alimpenda kweli hivyo jambo hilo lilimsumbua na kumtesa kiasi cha kumfanya kuandika wimbo huo na kurekodi. 

"Wimbo huu wa 'No Stress' ni personal issue nakumbuka niliandika wimbo huu siku tatu baada ya mpenzi wangu kuniacha, kama unavyojua tena mapenzi yanaumiza sana hasa pale unapokuwa umependa kweli harafu mtu anakuja kukuzingua. kiukweli hii ilikuwa ni fisrt time kwangu kupenda kweli hivyo iliniuma sana na kama mnavyojua mapenzi yanaumiza" alisema Angel Marry