Joseph Mbilinyi 'Mr II Sugu' apata mtoto wa tatu 

Jumamosi , 10th Oct , 2020

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Joseph Mbilinyi maarufu kama Mr II Sugu, ametoa taarifa ya kupata mtoto mwingine na mkewe Happiness Msonga.

Joseph Mbilinyi na mkewe Happiness Msonga

Akitoa taarifa hiyo kupitia post aliyoiweka kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram Joseph Mbilinyi ameandika kuwa 

"Taarifa, mimi na familia yangu tunaendelea kumshukuru sana Mungu, asubuhi ya leo ametujalia kupata mtoto mwingine, amezaliwa kwenye Hospitali ya wazazi Meta Jijini Mbeya na tumempa jina la Freeman, asanteni"

Kwa sasa Joseph Mbilinyi ana jumla ya watoto watatu ambao ni Shawn na Freeman Joseph Mbilinyi akiwapata kwa mkewe Happyness Msonga, huku mtoto wake wa kwanza Sasha alimpata alipokuwa na mfanyabiashara Faiza Ally.