Jumatatu , 9th Jan , 2017

Zikiwa zimeshapita siku kadhaa toka kundi la Navy Kenzo waweze kuipeleka mtaani Album yao ya 'AIM' amabayo ina jumla ya ngoma 11 wasanii hao wameonyeshwa kusikitishwa na kuvunjwa moyo na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakizivujisha ngoma hizo

Aika

Watu waliowanyooshea vidole zaidi ni Bloggers ambao wamekuwa wakichukua nyimbo zao kwenye Album na kuziweka kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza kwenye kipindi cha Bongo fleva Top 20 Aika alisema kitendo cha baadhi ya watu hususani bloggers kuchukua nyimbo hizo kwenye album na kuziweka mitandaoni kinakuwa kinawavunja moyo kwani kinasababisha biashara yao kupunguza kasi na kuharibu mauzo ya album hiyo mtaani.

Mbali na hilo Aika alisisitiza kuwa anatambua bloggers huenda wanajua wana wa'support' kwa ku-upload nyimbo hizo kwenye mitandao ya jamii ili kusaidia album kuuzika lakini huenda wengine hawajui kile wanachofanya kinawaharibia wao soko la album yao mtaani.

Msikilize hapa wakati akipiga story na Greyson Gideon katika Bongo Fleva Top 20