Harmorapa kwenye 18 za Alikiba, awa mpole ghafla

Jumatatu , 29th Mar , 2021

Kwa mara ya kwanza msanii Alikiba amekutana na Harmorapa kwenye siku ya mwisho ya kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt John Pombe Magufuli huko Wilayani Chato, Mkoani Geita.

Picha ya pamoja ya Alikiba kushoto na Harmorapa upande wa kulia.

Kupitia video ya hapo chini inaonyesha Alikiba amemshika mkono msanii Harmorapa huku akimuuliza baadhi ya maswali ambayo yalimfanya Harmorapa kuonekana mpole na kuogopa wakati anaulizwa.

Aidha baada ya kumshika mkono Harmorapa Alikiba amesema "Sema Mungu mkubwa maana Magufuli alikuwa kama zawadi kwetu, huyu naye ni msanii Harmorapa ndiyo maana yupo hapa, halafu Magufuli alikuwa sisi ndio marafiki zake".

Zaidi tazama hapo chini kwenye video kuona Alikiba na msanii wa filamu Dokii wakumuuliza maswali hayo Harmorapa.