Jumatatu , 15th Mar , 2021

Msanii Harmorapa amepata kigugumizi kizito kutoa maelezo baada ya ku-post picha ya mtoto wa staa wa filamu hapa nchini Kajala Masanja aitwaye Paulah kwenye siku ya wapendanao Februari 14.

Kushoto ni msanii Harmorapa, kulia ni Paula mtoto wa Kajala

Akizungumzia hilo kwenye kamera za EATV & EA Radio Digital,  Harmorapa amesema amepost picha hiyo kwa ajili ya upendo na hakuna kingine ila anamuombea aendelee vizuri na masomo yake kwa sababu bado ni mwanafunzi.

"Ile ni akaunti yangu nipo huru kupost chochote ambacho najisikia ila nisimkwaze wala nisimtukane mtu, kwa hiyo ni upendo tu ulinifanya nipost ila simaanishi kwanza naomba tuiache kwanza hiyo mada naona imekaa sio ila cha msingi asome" amesema Harmorapa 

Zaidi tazama hapa chini akizungumzia hilo.