Harmorapa afunguka kuhusu mjengo wake mpya

Tuesday , 14th Mar , 2017

Msanii Harmorapa ambaye haishi kwa kiki mjini ameibuka na jambo jipya kwa kusema amenunuliwa nyumba kali ya kuishi maeneo ya mikocheni Jijini Dar es Salaam na uongozi wake unaomsimamia kazi zake.

Harmorapa

Chipukizi huyo alisema mpaka sasa hajafahamu kiasi kilichogharimu kutumiwa katika kununuliwa nyumba hiyo kwa kuwa yeye amepewa kama zawadi. 

“Yaah nimenunuliwa nyumba maeneno ya Mikocheni na boss wangu Irene Sabuka, nyumba ipo fresh inavyumba viwili na sitting room na bafu na kila kitu ambacho staa anastahili kumiliki na menejineti imeamua kufanya hivi ili niweze kuwa kwenye nyumba ya hadhi ya staa kama mimi”. Alisema Harmorapa

Kwa upande mwingine msanii huyo kupitia kipindi cha FNL ya EATV alibainisha baadhi ya mambo na kubainisha kuwa alianza kuchana tangu kitambo lakini muda wa kutoka ndiyo ulikuwa bado haujafikia kwake hivyo amewataka watu wampe -support kwakuwa yeye pia ni msanii kama wasanii wengine hapa Tanzania.

Harmorapa ndani ya FNL

“Harmorapa hatafuti kiki, harmorapa ni msanii kama wasanii wengine ambao wanaamini ni wasanii, nimeanza kufanya ‘game’ muda tu ila nafasi na muda ndiyo ulikuwa bado hujafika kwangu mimi kuonekana. Sasa hivi ndiyo ‘time’ yangu" - Alisema Harmorapa

Msanii huyo kwa sasa anatamba na video yake mpya inayoitwa 'Kiboko ya Mabishoo' 

Recent Posts

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko, akiongela kubainika kwa makontena yenye mchanga wa dhahabu 262 katika bandari ya Dar es salaam leo tarehe 25 Machi, 2017 Wengine katika picha ni maafisa wa TPA na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Bandari Ramadhani Mungi

Current Affairs
Makontena mengine ya mchanga wa dhahabu yanaswa

Mbwana Samatta (Kushoto) akimtoka mchezaji wa Botswana katika mchezo

Sport
Samatta aing'arisha Taifa Stars

Rais Magufuli

Current Affairs
Rais Magufuli ateua bosi mpya wa TRA

Dele Alli akioneshwa kadi nyekundu katika moja ya mechi za UEFA dhidi ya Gent

Sport
Arsenal, Dele Alli 'wapigwa rungu' na UEFA

Basila Mwanukuzi na Seki Kasuga

Current Affairs
Vijana CCM wajitokeza kwa wingi ubunge wa EALA

Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga

Sport
Mayanga aomba nguvu za mashabiki Taifa Stars