Jumapili , 14th Mar , 2021

Msanii Harmonize ni miongoni mwa wasanii waliohusika kwenye ngoma nyingi barani Afrika siku za karibuni, ambapo ndani ya wiki hii zimetoka ngoma mbili kutoka mataifa ya Ghana na Nigeria, Harmonize akiwa ameshirikishwa.

Harmonize akiwa na Small God

Ngoma hizo ni Falling For U ya msanii Blaqjerzee wa Nigeria ambapo humo ndani pia ameshirikishwa Mr. Eazi.

Ngoma hiyo inaonekana ilirekodiwa wakati ambao Harmonize alikwenda kwenye tamasha moja huko Gahana na kukutana na wasanii wengi akiwemo Wizkid.

Ngoma nyingine ni Marry Me akiwa ameshirikishwa na Small God wa Ghana. Video ya wimbo huo pia imeshatoka.

Harmonize amewashukuru wasanii hao kwa collabo hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram.

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

A post shared by KONDEBOY (@harmonize_tz)