Hakuna msanii ana heshima kama Darassa - Dudu Baya

Thursday , 12th Jan , 2017

Rapa mkongwe nchini Dudubaya amefunguka na kumwaga sifa za kutosha kwa Rapa Darassa na kusema katika wasanii wa Tanzania hakuna msanii mwenye heshima kama Darassa.

Darassa (Kushoto)

Amesema pia kuwa ule mstari uliombwa kwenye wimbo wake wa 'Muziki' siyo Kenge, siyo Simba, siyo Mamba ni fleva tu ya muziki.

Akiongea kwenye kipindi cha eNEWZ Dudu Baya amesema anampa big up Darassa kwani muda mrefu alikuwa anaimba muziki lakini hakuweza kutoboa lakini saizi amefanya ngoma yake ya Muziki na kutoka vizuri mpaka kukubalika kwa watanzania.

"Darassa ni mdogo wangu ameanza kuimba muda mrefu sana lakini saizi ndiyo ametoboa, kile alichoimba sijui siyo Kenge siyo Simba siyo Mamba zile ni fleva tu za muziki amepiga mistari na mimi ngoma yake nai support. Lakini niseme tu hakuna msanii mwenye heshima kama Darassa narudia tena hakuna msanii mwenye heshima kama Darassa" alisisitiza Dudu Baya 

Recent Posts

Mch. Anthony Lusekelo

Current Affairs
Mzee wa Upako afunguka kuhusu yeye kunywa pombe

Shamba la bangi tayari kwa kuteketezwa, huku mtuhumiwa wa kilimo hicho akiwa chini ya ulinzi (Picha: Maktaba)

Current Affairs
Ukikutwa na shamba la bangi, jela miaka 30

Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiambatana na Waziri Charles Mwijage kukagua eneo ambapo kitajengwa kiwanda cha vigae.

Current Affairs
Kikwete 'alivyopora dili' la kiwanda cha vigae