Jumatatu , 21st Sep , 2020

Msanii asiyeishiwa na vituko hapa nchini Gigy Money ameonekana akipima ugonjwa wa Ukimwi Live kupitia Insta Story yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram na vipimo vyake vimeonyesha kuwa yupo salama.

Msanii wa muziki na filamu Gigy Money

Akipost video fupi kwenye mtandao wa Instagram ikimuonyesha anapima ugonjwa huo kwenye moja ya hospitali Gigy Money amesema haogopi kwa sababu anajiamini kuwa hawezi kuwa na ngoma wala ujauzito.

"Sina mimba wala ngoma tena napima hapa mbele ya nesi dunia yangu hii, mimi mama Mayra nipo salama najipenda na najikubali kupima Ukimwi ni bure ila siwezi kuwa mgonjwa, maana akili yangu tupu inaumwa, tena hapa nachukua vipimo vingine nampelekea mpenzi wangu na yeye akapime, kupima bure na Ukimwi upo" amesema Gigy Money 

Lingine kuhusiana na Gigy Money kupitia mitandao ya kijamii ameonekana akipigana na msanii mwenzake Zee Cute kwenye moja ya matukio yaliyofanyika jana usiku.