Alhamisi , 16th Feb , 2017

Rapa Fareed Kubanda amemsainisha msanii Big Jahman kwenye label yake ya Cheusi dawa Entertainment na kuanza kumsimamia kazi zake

Akiongea kwenye kipindi 5Selekt kinachorushwa na ting'a namba moja kwa vijana Big Jahman anasema yeye mwenyewe alimfuata Fid Q na kumuomba amsimamie kazi zake kwani lengo lake lilikuwa ni kurudi kufanya vyema na kufanya biashara katika muziki. 

Big Jahman akiwa chini ya usimamizi wa Fid Q ameachia kazi yake ya kwanza inayoitwa 'Mabundi' akiwa ameshirikiana na Fid Q mwenyewe pamoja na Saraha.

Itazame....