Ijumaa , 15th Sep , 2017

Msanii mkongwe wa bongo fleva Dudubaya ameanza kujirudi na kumsifia rapa mwenzake Chid Benz kwa kuweza kukabiliana na hali aliyokuwa nayo awali ya matumizi ya dawa za kulevya.

Dudubaya ameeleza hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kupita siku kadhaa tokea atoe kauli yake iliyokuwa imejaa utata juu ya msanii mwenzake Chid Benz kwa kusema ni bora aachwe asisaidiwe  jambo lolote kwa kuwa kifo ndicho kinamsubiri na kusababisha watu wengi waamini wawili hao hawako sawa kutoka na jambo hilo.

"Suala la msingi kwa sasa nampa 'big up' Chid Benz kwa kuwa ameweza ku-recover katika hali yake, pia namsifu kwa kuweza kuitumia 'mic'  vizuri na pumzi ya kutosha. Sina mashaka naye, namkubali sana ila mimi kama kaka yake namsisitizia tena, sitaki nimemuone anarudi kule alipokuwa ameangukia, Mungu amuinuie na amsimamie", amesema Dudubaya.

Tazama hapa uone anavyofunguka zaidi Dudubaya kuhusu Chid Benz na hali yake ya sasa.