Dogo Mfaume afariki dunia

Wednesday , 17th May , 2017

Msanii wa muziki wa bongo fleva, Dogo Mfaume ambaye aliwahi kutamba na nyimbo kama 'Kazi Yangu Ya Dukani' amefariki dunia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akiendelea kupatiwa matibabu. 

Msanii Dogo Mfaume enzi za uhai wake.

Dogo Mfaume ambaye alitumbukia kwenye janga la madawa ya kulevya na baadaye kuanza kupata matibabu ya kuondokana na matumizi ya madawa hayo kupitia kituo cha "Back to Life Sober House" kinachoendeshwa na  Pilli Missana kilichopo Kigamboni Dar es Salaam. 

Akiongea na EATV Pili Missana ambaye ni Mkurugenzi wa kituo hicho amethibitisha kufariki kwa msanii huyo huku akisema alikuwa amelazwa Muhimbili kwa matibabu, kabla ya umauti kumkuta. 

Mungu amlaze mahali pema peponi Dogo Mfaume. Jikumbushe na moja ya kazi yake hapo chini 
 

Recent Posts

Rais Magufuli

Current Affairs
Tanzania kuzalisha Megawatts 10,000 za umeme

Golden State Warriors Vs San Antonio Spurs

Sport
Warriors yatinga fainali, yaweka historia NBA

Kamishna Simon Sirro

Current Affairs
Tutakupoteza ukiwa bado mdogo - Sirro

Katibu mkuu Yanga, Charles Boniface Mkwasa

Sport
Kombe la Yanga kutua Bungeni

Muonekano wa ziwa Victoria (Picha: Maktaba)

Current Affairs
Wanafunzi watatu wafa maji Geita
Entertainment
Mzee Yussuf aibuka