Jumatano , 28th Oct , 2020

Leo ni Oktoba 28 ni siku ambayo wananchi wa Tanzania wanapata nafasi ya kuchagua viongozi watakaowaongoza kwenye miaka mitano ijayo kuanzia Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Picha ya kati ni Faiza Ally, kulia ni Dogo Janja, kushoto ni kitambulisho alichotumia msanii wa filamu Riyama Ally

Hawa hapa ni baadhi ya mastaa ambao tayari wameshapiga kura kwenye vituo vyao walivyojiandikishia ambapo wameshea picha, video na maandishi kwenye mitandao yao ya kijamii zikiwaonyesha wameshamaliza kufanya tukio hilo ili kuhimiza watu wengine wakapige kura.

"Nimepiga kura, Uchaguzi wa amani Tanzania" msanii Quick Rocka 

"Ni haki yako usiipoteze, piga kura" msanii Dogo Janja 

"Nimepiga kura, nina furaha nimejipa haki yangu, sehemu za uchaguzi ziko salama sana, nimefurahi kuona amani na utulivu kila nilipopita, Mungu naomba endelea kutupa amani katika nchi yetu, naipenda Tanzania yangu" Mfanyabiashara Faiza Ally 

"Alhamdulilah nimeshatimiza wajibu wangu, nawaombea mashabiki zangu na marafiki zangu uchaguzi mwema, tukimaliza kupiga kura turudi nyumbani kufuatilia matokeo katika TV na Radio, mimi nipo hapa sebuleni nafuatilia matokeo, Tanzania yetu, amani yetu, urithi wetu" msanii wa filamu Riyama Ally 

"Nimetimiza haki yangu ya msingi" msanii Madee Seneda 

"Nimefurahi sana nimetimiza haki yangu ya msingi" msanii Shilole