Dogo Janja alinificha sana - Madee

Sunday , 5th Nov , 2017

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Madee amefunguka na kusema kuwa msanii Dogo Janja ambaye amemlea na kumtambulisha katika ulimwengu wa muziki alimficha sana kuhusu mahusiano yake na Irene Uwoya. 

Madee amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Friday Night Live (FNL) na kudai kuwa awali kabla ya kupewa taarifa ya msanii huyo kuoa walikaa karibu siku mbili wakijifikiria wanapelekaje taarifa hizo kwake na kusema siku alipoambiwa hakuamini hivyo ilibidi ampigie simu Irene Uwoya kwanza kutaka kujua kama kweli au Dogo Janja anataka kumpiga mzinga. 

Mtazame hapa Madee akifunguka zaidi