Alhamisi , 16th Feb , 2017

Ikiwa mpaka sasa imepita zaidi ya miezi miwili tangu rapa Darassa alipoachia wimbo wake wa 'Muziki' na kufanikiwa kupata mafanikio makubwa zaidi kuliko wakati wote katika muziki wake rapa huyo ameonekana kuwachanganya mashabiki zake juu ya kazi mpya.

Darassa

Darassa aliweka ujumbe akisema anaangalia mafanikio ya kazi zake za nyuma kabla ya kuachia ngoma nyingine kisha akawauliza mashabiki kama wapo tayari kwa kazi mpya au bado na ndipo hapo alipoanza kuwachanganya huku wengine wakishauri atulie kwanza muziki iendelee kufanya poa na wengine wakimshauri kuwa ni muda sahihi yeye kuachia ngoma mpya.

Baaadhi ya mashabiki wa Darassa wameonesha wasiwasi kuwa huenda msanii huyo akashindwa kuleta ngoma ambayo inaweza kufanya vyema kama kazi yake ya muziki.

Tazama hapa...