Jumanne , 27th Sep , 2022

Captain wa BongoFleva msanii Danzak amekana taarifa za kuwa kwenye mahusiano na staa wa filamu Bongo madama Wema Sepetu kwa kusema ni mtu wake wa karibu.

Picha ya Wema Sepetu na Danzak

Akiweka wazi taarifa hizo za ku-date na Wema Sepetu kupitia Friday Night Live ya East Africa TV na East Africa Radio Danzak amesema 

"Wema ni mwanangu sana, mshkaji wangu na rafiki yangu sana. Sijui kwanini wananiita mimi shemeji wa Taifa mnanipa kesi tu ila nampenda na historia yake ina-inspire sana".

Kwa sasa staa huyo wa filamu Wema Sepetu inasemekana yupo penzini na msanii Whozu.