Jumapili , 27th Sep , 2020

Msanii wa Rap, Bongo, Chidi Benzi, amefunguka kuhusu upendo alionao kwa baba yake ambapo amesema hata akimfanyia kosa gani kwakwe yeye haoni kama ni kosa.

Chidi Benzi.

Akifunguka kupitia (Friday Night Live) ya East Africa TV ameeleza kuwa hakuwahi kukaa karibu sana na mzazi wake wa kiume ila hiyo haimaanishi kutokumjali kama baba.

"Uwepo wa baba yangu kwangu sioni kosa kabisa natamani nipate kingi nimgawie kidogo sioni kama anastahili adhabu yoyote hata kama alimzingua mama"amesema Chidi Benzi

"Tunaonga kichizi huwezi kushindwa kumhudumia mzazi wako hakuna ulazima wa kumchukia baba hata kama kafanya chochote kile ,wapo watu wenye matatizo na baba zao ila nawashauri tu kwa mtoto wa kiume haijalishi kafanya nini baba yako mpende tu ni mzazi wako".