Jumanne , 29th Sep , 2020

Mapema kabisa siku ya leo Septemba 29, zimetoka taarifa kuhusu kifo cha mpiga gitaa la solo wa bendi ya Msondo Ngoma Said Mabera, ambaye amefariki kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Marehem Said Mabera enzi za uhai wake

Mzee Said Mabera ambaye amefanya kazi katika bendi hiyo kuanzia mwaka 1973, anatarajiwa kuzikwa leo nyumbani kwake maeneo ya Goba "Tegeta A" na mazishi yatafanyika kuanzia saa 10:00 jioni. 

Kupitia mahojiano ya EATV & EA Radio Digital ambayo tumefanya na mtangazaji Zomboko wa ITV amesema kuwa, chanzo cha kifo chake ni magonjwa ya uzee na umri, kwa sababu kabla ya hapo alikuwa anasumbuliwa na magonjwa hayo kwa kipindi cha miezi mitatu nyuma.