Bongo Movie tunawajua zaidi kwa mengine - Nikki

Friday , 21st Apr , 2017

Rapa Nikki wa Pili kutoka katika kundi la Weusi amefunguka na kusema kuwa wasanii wengi wa bongo movie wanafahamika kwa mambo mengi na si kufahamika zaidi kutokana na kazi zao za kila siku.

Nikki wa Pili

Nikki alisema hayo kama kuwapa funzo wasanii wa filamu kuwa wanapaswa kufanya kazi ambazo ndiyo zitawapa heshima zaidi na kuwafanya watu watambue kazi zao kuliko mambo mengine.

Amekiri kuwa mwanzo wasanii wa bongo movie walifanikiwa kupata soko zuri la kazi yao na kazi kukubalika zaidi kutoka na ukweli kwamba kipindi hicho huenda walikuwa wanafanya kazi ambazo zilikuwa na tija kwa wananchi.

"Bongo movies mwanzoni walikuwa na soko, kuanza ni kujaribu,  ila ku-sustain is a science... mwendelezo wa lolote huhitaji maarifa. Movies za Rambo ni maarufu kuliko Rambo mwenyewe, bongo movies tunawajuwa kwa vitu vingine zaidi wala hata siyo movie zao". Alisema Nikki wa Pili 

Mbali na hilo Nikki alikwenda mbali zaidi na kusema kuna maisha ya baadhi ya waigizaji wa Tanzania wanayoishi hupelekea kundi la watu fulani kutofuatilia kabisa movie zao kutokana na aina ya maisha ya waigizaji hao, Nikki anadai hakuna uhusiano wowote katika maisha yao na kazi zao jambo ambalo linapelekea watu kushindwa kuamini hata vile wanavyo igiza katika filamu zao.

"Kuna aina ya maisha wanaishi baadhi ya waigizaji, itakuwa ngumu sana kwa watu fulani kuangalia movies zao, nampenda Denzel kwenye movie na kwenye maisha ya kawaida, kwenye interview, kwenye speech, anajua kukufanya uamini movie zake" alisema Niki wa Pili 

Recent Posts

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa

Current Affairs
Marufuku kusafirisha chakula nje - Majaliwa

Mshambuliaji wa kimataifa anayeitumikia klabu ya Dhofar SC ya nchini Oman, Elias Maguli.

Sport
Wachezaji bongo tusiogope kwenda nje - Maguli

Mlinda mlango wa Azam FC na timu ya taifa ya Tanzania Aishi Salum Manula.

Sport
Sijasaini mkataba Simba - Aishi

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo

Current Affairs
Kufa maskini ujinga - Mzee wa Upako

Waziri wa Mambo ya ndani , Mwigulu Nchemba.

Current Affairs
Mwigulu Nchemba aibua vita ya ushoga