Jumatatu , 19th Jun , 2017

'Hit maker' wa ‘Mazoea’, Billnass amefunguka kwa kusema hajafurahishwa kuhusishwa kwenye ugomvi unaoendelea baina ya msanii Godzilla na Wakazi kwa kudai kitendo hicho kinaweza kumsababishia mashabiki kutomuelewa. 

Msanii Billnass

Billnas amesema hayo siku moja kupita baada ya bifu ya wasanii hao kuzidi kushika kasi katika vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii.

"Sijui bifu yao imeanzia wapi au inahusu nini lakini nimesikia namna walivyonihusisha 'sometimes' siyo kitu kizuri sana kwa sababu ukisema Godzilla ana-stress halafu Billnass ndiyo anamsababisha unahisi mashabiki wa Godzilla wakiniona mimi si watasema huyu ndiyo kikwazo cha msanii wetu asifike mahali, kumbe kila mtu anachangamoto zake" alisema Billnass.

Pamoja na hayo Bill aliendelea kufunguka kwa kusema haamini kama Godzilla atakuwa na mawazo ambayo yamempelekea kugombana na wasanii wenzake.

"Mimi siamini kama Godzilla ana 'stress', kwasababu Godzilla ni kati ya watu waliofanya vizuri kwa mfululizo, ana matukio mengi, ana mizizi kwenye huu muziki na bado ana nafasi kubwa kwenye hii tasnia” alisisitiza Bill