Jumanne , 10th Jan , 2017

Mwanamuziki Ben Pol anayekiki na ngoma yake ya 'Phone' amefunguka na kuweka wazi mipango yake ndoa na kusema kwa sasa yeye kuoa bado kwani anataka kujipanga zaidi lakini pia hata ikifika wakati wa kuoa itabidi aoe kimyakimya ili kulinda 'career' yake

Ben Pol

Ben Pol amesema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema hata ikifika wakati wa kuoa ataoa kimya kimya kwani anaogopa asijekupoteza mashabiki zake kwenye muziki ambao huwa wanajipa moyo kupata nafasi hiyo.

"Mimi kuoa bado kidogo nafikiri itafika muda muafaka nitafunga ndoa, bado najipanga ila mimi naamini ndoa huwa ina tabia ya kuharibu career kidogo kwa asilimia kadhaa. Hivyo nitaoa kimya kimya kwa sababu sisi tuna mashabiki wengi na wengine wanaona huenda kukawa na nafasi kwao sasa ukioa wakajua unaweza kuwakosa hao kwenye muziki wako" alisema Ben Pol