Jumanne , 21st Feb , 2017

Msanii wa bongo fleva Ben Pol amesema anatamani sana kuwasaida baadhi ya wasanii ambao wapo level za chini na anatamani kuwa'push' ili wafike level za juu zaidi kwenye 'Game' hapa bongo, lakini hana uwezo huo kwa sasa.

Ben Pol

Ben Pol akiwa kwenye Planet Bongo ya EATV amewataja wasanii Ibrah Nation, Foby pamoja na  Ivra kuwa ni kati ya wasanii ambao anatamani kuwasaida ili kuwavusha kwenye level za juu zaidi kimafanikio.

“Unajua huwezi kusema wazi kuwa unataka kumsaida mtu fulani maana sio kila mtu anahitaji msaada kama unavyodhani ila mimi nadhani kama ni kuwasaida basi ningewasaini Ibrah Nation, Ivra na jamaa mmoja hivi kaimba nyimbo ya mimi ni staa nadhani anaitwa Foby hivyo nadhani hao ndiyo ninaotamani sana kuwasaidia”. Alisema Benpol

Aidha msanii huyo ameweka wazi kuwa Rappa Hamorappa alimpigia simu wiki mbili zilizopita hivyo kitu chochote kinaweza kutokea kuanzia sasa.