Jumatano , 22nd Feb , 2017

Msanii wa bongo fleva Barnaba Classic ameeleza nia yake ya kuja na albam yake ya nyimbo nane na jinsi ya usambazaji wake utakavyokuwa tofauti na ule watu wengi waliouzoea, huku akiweka pia wimbo wa dini kwenye albam hiyo.

Barnaba

Akiongea kupitia eNewz Barnaba amesema  "Nina mpango wa kutoa albam tarehe nane mwenzi wa nane yenye jumla ya nyimbo kumi, ambapo kati ya hizo nyimbo kumi, Love Boy itakuwa ndani na nyimbo moja itakuwa ya dini na nyimbo nyingine itakuwa bonasi ya mashabiki zangu" alisema Barnaba

Hata hivyo Barnaba alisema albam yake itaitwa 'Lover Boy' kwa kuwa huo ndiyo wimbo wake uliofanya vizuri kwa mwaka 2016 ingawa ana mpango wa kuachia nwimbo  mwingine kabla ya mwenzi wa nane kama mambo yake yakikaa sawa .

Mtazame katika video hii alipozungumza na kipindi cha eNewz cha EATV