Ijumaa , 17th Feb , 2017

Msanii wa bongo fleva Barnaba amemuomba msamaha Ice Boy kwa kumcheleweshea mafanikio katika  muziki wake, kama Ice Boy mwenyewe alivyowahi kudai.

Barnaba Classic

 

Akiongea kupitia eNewz ya EATV, Barnaba amesema  "Naomba tena radhi kwa jamii kwa kauli ya Ice aliyosema kwamba mimi ndiye nimemchelewesha kufanikiwa katika muziki wake kwa kuwa sipendi kugombana na kukwanzana na mtu namuomba radhi kupitia eNewz kwamba anisameha kwa makosa yangu" alisema Barnaba

Hata hivyo Barnaba alisema siri ya mafanikio siyo kuvaa vizuri, kula vizuri au kuishi pazuri bali ni kuwa na heshima na kuepukana na malumbano na ugomvi usio wa lazima.

Mtazame hapa katika eNewz