Ijumaa , 10th Nov , 2017

Mpiga picha maarufu bongo ambaye pia ni meneja wa baadhi ya wasanii hapa bongo Mx Carter, amejibu tuhuma za msanii Baraka The Prince kuhusu kuchezea acount yake ya YouTube na kupunguza namba za watazamaji.

Akiongea kwenye eNewz ya East Aftica Television, Mx Carter amesema anahisi Baraka ana stress hivyo anahitaji msaada, kwani anayoyafanya yanawashangaza watu.

Mx Carter ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya mitandao, amesema Baraka mwenyewe alimfuata kumuomba amfutie account yake ya kwanza ambayo ilikuwa chini ya uongozi wake wa zamani wa RockStar 4000, kwa kuwa hakuwa akiwaamini watu hao na kuwahisi kumfanyia kitu kibaya.

“Baraka haeleweki alinifuata nimsaidie nikamsaidia akaenda kufanya interview kila media anayoenda anaongea tofauti, hata ukiangalia coment nyingi za watu ambao wamesikia interview wameshindwa kuelewa ana kitu gani kinamchanganya, ananiomba msamaha kwamba amekosea hakujua nini anafanya, nahisi ana stress tunaweza tukakaa chini kumshauri nini cha kufanya”, asema Mx Carter.

Mx Carter ameendelea kwa kusema kwamba na sio yeye peke yake ambaye amemtuhumu, kwani sasa hivi amehamishia balaa kwa msanii mwenzake Shilole, akisema ndiye aliyemwambia kwamba Mx Carter ameichezea acount yake.

“Sasa kama anagombana na watu kwa style hii hata akija tena siwezi kumsaidia kwa 100%, na hapa ninavyokwambia tayari kashaanzisha mtiti sehemu nyingine, akasema Shilole ndio kamsababisha aseme hivyo, sasa hivi hapatani na Shilole, kwa mantiki hiyo Shilole hawezi kumpostia video yake”, amesema Mx Carter.

Kutokana na hayo yote Mx Carter amesema kitendo cha mtu kupunguza namba za watazamaji YouTube ni kitu ambacho hakiwezekani, kwani kufanya hivyo inamaana unaingia kwenye 'server' za Youtube, kitu ambacho hakiwezekani.