Jumamosi , 15th Mei , 2021

Masta AY ameitabiria mema Album ya Producer Marco Chali iitwayo ONA ambayo itatoka siku ya Mei 28 kwa kusema ni Album  Classic na nyimbo zake zitaishi kwa muda mrefu sana kwa sababu ya ujumbe uliopo kwenye nyimbo hizo.

Kulia nim msanii AY, kushoto ni Producer Marco Chali

"ONA Album mpya ya Marco Chali inakuja mwezi huu, hii ni kati ya Album classic kabisa nayotabiri kuwa nyimbo zake zitaishi kwa kipindi kirefu sana kutokana na jumbe tofauti zilizoimbwa humo, stay tuned" ameeleza AY

Pia mwaka huu tegemea Album zingine kutoka kwa wasanii ambao wameahidi kama Prof Jay, Alikiba, Harmonize, Killy, Cheed, Country Boy, Moni Centrozone na wengineo.