Alhamisi , 14th Sep , 2017

Msanii Ney Wamitego amefunguka kujibu kauli iliyotolewa na Balozi Getrude Mongela kwamba wanaume siku hizi hawajui kutongoza ndio sababu wanabaka, na kusema kuwa jambo hilo halina ukweli wowote.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Ney amesema mambo ya kutongozana kwa miaka ya sasa hivi hakuna, kwani hali imebadilika kabisa ambapo ukimtaka mwanamke ni mnawasiliana kwa ishara tu na kumalizana.

Ney ameendelea kusema kwamba hata watu wanaofanya vitendo vya ubakaji sio kwa sababu hawajui kutongoza, isipokuwa ni ufinyu wa mawazo yao na tamaa.

Msikilize hapa chini