AUDIO: "Baraka nitakuharibia zaidi". - Shilole

Friday , 10th Nov , 2017

Msanii Shilole ambaye ametajwa kuhusika kwenye sakata la Baraka the Prince na Mx Carter, amemjia juu Baraka The Prince na kumtaka asimuhusishe kwenye matatizo yake, kwani atamuharibu zaidi.

Akiongea na mwandishi wa habari wa East Africa Television website, Shilole amesema hakuzungumza na Baraka kuhusu kitu chochote zaidi ya kumuomba ampostie wimbo wake, hivyo anashangaa kwa kitendo cha Baraka kumwambia Mx Carter kwamba yeye ndiye aliyemwambia kwamba anahusika na kuharibu YouTube ya Baraka.

Msikilize hapa chini akitoa povu la nguvu kwa Baraka