Jumatatu , 24th Jul , 2017

Barnaba Classic amefunguka kwa kudai sehemu kubwa ya tungo ya nyimbo zake anazoimba yeye pamoja na wasanii wengine huwa ni mambo ya kweli ambayo yamewatokea wao ama watu wao wakaribu.

Msanii Barnaba (Kushoto) akiwa na mtangazaji wa kipindi cha Bongo flava Top 20 Jr. Junior

Barnaba amebainisha hayo katika kipindi cha Bongo flava Top 20 kutoka East Africa Radio ambapo ilikuwa live kutokea viwanja vya Don Bosco Oysterbay Jijini Dar es Salaam na kusema kwa upande wake haoni faida ya kuachia nyimbo mara kwa mara kama wanavyofanya baadhi ya wasanii wachache wenye lengo la kuharibu kazi za wenzao mpya zinaachiwa.

"Tunachokiimba ni 'reality' yaani karibu asilimia 75 ya nyimbo zangu ni mambo ambayo yamenitokea mimi pia muda mwingine ni kuutoka kwa rafiki zangu pamoja na jamii inayonizunguka. Pia namuunga mkono Shetta kwa suala lake aliloongea hivi karibuni kuhusiana na kutoa nyimbo kwa mfululizo kwa upande wangu sioni manufaa ya aina yeyote katika hilo", amesema Barnaba.

Kwa upande mwingine Barnaba amesema yupo mbioni naye kutengeneza T-shirt zenye jina lake lengo ni kutaka kuwafurahisha mashabiki zake waliyokuwa wakiomuomba kwa kipindi kirefu.