Jumatatu , 26th Oct , 2020

Meneja, msanii wa filamu na producer wa muziki Max Rioba amefunguka suala kumvuta msanii Alikiba kwenye filamu ambapo atakuwa kwenye tamthilia yake na tayari ameshamwambia msanii huyo vitu vikikaa sawa watafanya mambo.

Kwenye picha kubwa ni msanii Alikiba, picha ndogo ni meneja Max Rioba

Kupitia EATV & EA Radio Digital tumefanya mahojiano na wote wawili ili kuzungumiza hilo ambapo Max Rioba amefunguka kuwa 

"Natamani kufanya kazi na Alikiba na tayari nimeshazungumza naye tayari kuna mipango ambayo tunaiweka sawa na tutafanya kazi pamoja kuanzia kuandika wimbo, kutoa nyimbo, collabo na awe kwenye tamthilia yangu"  

Aidha kwa upande wa msanii Alikiba amesema "Max Rioba ni mtu mwenye 'vision' tofauti ndiyo maana namkubali katika hilo, hata kwenye video yangu ya mvumo wa radi alifanya kitu, hivyo wategemee kwamba naweza kufanya naye kazi muda sio mrefu, pia nishafanyaga filamu kipaji hicho kipo na nilianzia shuleni na sanaa tunaishi nayo".

Meneja Max Rioba tayari ameshafanya kazi na wasanii wakubwa hapa Bongo kama Wema Sepetu, Hamisa Mobetto, Shilole na Young Dee.

Zaidi tazama kwenye video hapa chini