Jumatano , 24th Mei , 2017

Msanii wa filamu nchini, Jacqueline Wolper amefunguka na kusema endapo mwaka (2020) Mh. Edward Lowassa atagombea Urais basi yeye atajitoa moja kwa moja kumsapoti katika kampeni zake kwani yeye ni shabiki mkubwa sana wa Waziri huyo Mstaafu.

Wolper amesema hayo kupitia kipindi cha KIKAANGONI kinachofanyika kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV na kudai kuwa yeye anampenda sana Lowassa pamoja na mkewe na kusema hata kampeni za mwaka 2015 alijitoa kumsapoti Lowassa kutokana na mapenzi yake kwani hakuwahi kulipwa hata elfu kumi.

"Kama Edward Lowassa atagombea urais mwaka 2020 Mungu wangu nitampa sapoti yangu moja kwa moja, mimi nampenda sana Lowassa na mkewe na nilianza kumpenda Lowassa toka kanisani maana kila harambee alikuwa anakuja, kwa hiyo mimi ni shabiki wa Lowassa na mkewe nilifanya kampeni kwa ajili ya kumsapoti Mh. Lowassa na sijawahi kuchukua pesa yoyote lakini watu wake walinitelekeza ndiyo maana nilikwenda CCM" -alisema Wolper.

Hata hivyo Wolper ambaye alionekana kuwa na ushawoshi mkubwa kwenye kampeni za 2015 anadai baadaye aliamua kwenda CCM sababu huko kulikuwa na rafiki zake wengi na watu wa huko walikuwa wakimjali tofauti na CHADEMA.