Jumanne , 1st Dec , 2020

Katika kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani uwepo wa mitaala itakayosaidia utaoaji wa elimu ya uzazi kwa watoto umetajwa kuwa utasaidia katika kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI nchini.

Mwalimu akielezea jambo wanafunzi (Picha kutoka mtandaoni).

Hayo yamesemwa na Afisa Sheria, Kutoka Chama cha Wanasheria Wanawake nchini (TAWLA), Joseph Oguda, akiwa katika kipindi cha Supa Breakfast ambapo amesema  kwa mujibu ya utafiti wa TAKUKURU ongezeko la maambukizi mapya ya virusi hivi yamechangiwa na rushwa ya ngono iliyosheheni vyuoni.

“Mtaala wetu wa elimu haujahusisha mtaala wa elimu ya uzazi ambapo watoto walitakiwa wapewe elimu ya uzazi kuwajengea msingi na ili kuweza kujiepusha na athari ukatili wa ngono , elimu zinatolewa na asasi kila siku lakini bado kuna chanagmoto ya utayari wa jamii inayopewa hiyo elimu” amesema Oguda

Aidha Oguda ameweka wazi kuwa bado kuna changomoto kwa upande wa vijijini na sehemu chache za majini kwa upande wa mila na desturi ambazo zinachangia katika kuongeza maambukizi ya virusi hivi.

“Umaskini unachangia watu kujihusisha na ngono, kwa maeneo ya Pwani mila na desturi potofu zilizopitwa na wakati zimechangia maabukizi ipo imani kuwa ukifanya mapenzi na mtu ambaye hajafikisha miaka 18 unapona VVU , na kwa Tarime kuna mila msichana awezi kuwa msichana jasiri pasipo kukeketwa hivyo wanajiweka katika hatari ya kupata virusi vya Ukimwi” amesema Oguda