Jumatatu , 20th Nov , 2017

Mbunge wa Kigoma mjini Mh. Zitto Kabwe amesema anajipanga kulifunguliwa kesi ya kikatiba jeshi la polisi nchini kutokana na kushikilia simu yake.

Zitto ameeleza kuwa Simu yake inashikiliwa tangu 7/11/2017 alipokamatwa kwa tuhuma za kuvunja sheria ya takwimu pamoja na sheria ya makosa ya mtandao.

“Walisema watahitaji simu hiyo kwa siku 2 tu, nilikwenda polisi KAMATA siku 3 baadaye nikaelezwa kuwa bado wanaendelea na uchunguzi. Nimerudi leo tarehe 20/11/2017, Polisi wanasema bado wanahitaji simu yangu hiyo”, amesema Zitto.

Kiongozi huyo wa chama cha ACT-Wazalendo ameongeza kuwa, “Nimeamua kuwaachia Simu mpaka hapo watakapotosheka lakini wajiandae na kesi ya kikatiba ambayo pia italinda haki za wananchi wengi wanaothirika na matumizi mabaya ya sheria ya Mtandao ( Cybercrime Act )”.