Ijumaa , 23rd Jun , 2017

Rais wa Tanzania John Magufuli, amemaliza ziara yake ya siku 3 Mkoani Pwani kwa kumuagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage kuwanyang’anya viwanda watu wote waliouziwa viwanda na Serikali na baadaye kuvitelekeza

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage

Mhe. Rais Magufuli amesema kuna viwanda 197 ambavyo viliuzwa kwa watu mbalimbali kwa lengo la kuviendeleza lakini viwanda hivyo vimekufa na vingine kubadilishiwa matumizi na kwamba jambo hilo linarudisha nyuma juhudi za kutekeleza mpango wa ujenzi wa viwanda na kyuongeza wapatiwe watu wengine watakaoweza kuviendeleza.

Mhe. Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo baada ya kuweka jiwe la msingi katika kiwanda cha kusindika matunda Wilayani Chalinze ambapo pindi kitakapokamilika kitakuwa na uwezo wa kusindika tani 300 za matunda kwa siku, kuajiri wafanyakazi 800 na kitawanufaisha wakulima 30,000.