Jumatatu , 28th Sep , 2020

Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein amesema kuwa wameamua kujitegemea wenyewe kwenye mambo ya msingi badala ya kutegemea mikopo.

Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa Terminal III ya Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume Kisauni,leo Septemba 28, amesema mradi huo umelipiwa na fedha za ndani na hawajakopa pahala popote.

"Kwahiyo sasa ndugu wananchi tumeamaua tunajitegemea wenyewe kwenye mambo ya msingi lazima tufanye wenyewe hii kukopakopa wakati mwingine tunachelewesha maana mpaka wakubali wenyewe ndo watukopeshe" alisema Dkt.Shein

Aliendelea kufafanua, "Lakini tukipanga vizuri bajeti yetu wenyewe tutafanya mambo mengi sana, tumeonyesha njia miaka miwili iliyopita” alisema Dkt.Shein

Leo Dkt. Shein alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Terminal III ya Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume .