Jumatatu , 20th Nov , 2017

Watu ambao hawajajulikana wamechimba mtaro na kutokea kwenye 'strong room' ya benki ya KCB tawi la Thika nchini Kenya, na kuiba shilingi milioni 50 za Kenya ambazo ni sawa na Bilioni 1.1 za Tanzania.

Tukio hilo ambalo limethibitishwa na Meneja wa Benki hiyo kwenye kituo cha Polisi cha Thika, Samuel Nganga, limetokea leo asubuhi majira ya saa 2:30 asubuhi alipoenda kufungua chumba hiko na kukuta kumevunjwa na kuibwa kiasi hiko cha pesa ambacho kilikuwa kwenye shelf mbili.

Polisi walifika eneo la tukio na kukuta eneo hilo likiwa limekatwa kitaalam zaidi, na kuhisiwa kuwa huenda walitumia kifaa maalum cha kuunguzia (oxy-Acytelene flame).