Jumanne , 26th Sep , 2017

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage leo amezindua Bodi mpya ya Kituo cha Uwekezaji (TIC) na tovuti ya jijini Dar es Salaam.

Katika uzinduzi wa Bodi hiyo, Mwijage amesema kuwa Wizara inaendelea kupambana kuondoa urasimu ambapo tayari imeanzisha kamati ya kitaifa ya kuhudumia wawekezaji na wajumbe ni taasisi zote zinazotoa huduma kwa wawekezaji.

Waziri ameongeza kuwa hadi sasa matokeo ni mazuri na wameanza kupata ripoti zikipongeza juhudi za kuondoa urasimu kwenye utoaji wa vibali na leseni mbalimbali nchini.

Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Uwekezaji (TIC) Profesa Longinus Rutasitara, amesema kuwa, Bodi itatoa ushirikiano kuhakikisha majukumu ya TIC yanatimizwa ipasavyo.