Waziri wa Maendeleo ya Jamii Dkt. Dorothy Gwajima
Akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Town iliyopo Manispaa ya Shinyanga Waziri Dkt. amesema jukumu la kuwalinda watoto ni la kila mmoja huku akiwataka wadau wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kuendelea kupaza sauti.
Katika hatua nyingine Dkt. Gwajima akatoa maelekezo kwa Halmashauri zote nchini kuandaa mifumo ya pamoja itakayoshirikisha wadau kupata taarifa haraka za ukatili kwa watoto.