Jumamosi , 27th Feb , 2021

Naibu Waziri wa Maji Maryprisca Mahundi, ametoa siku 7 kwa mkandarasi Petty Construction, kurudisha pampu ya kusukumia maji aliyoiondoa baada ya kunyang'anywa mradi wa maji wa Nyamtukuza uliokwama kwa miaka saba na kusababisha adha ya maji wilayani Nyang'hwale.

Naibu Waziri wa Maji Maryprisca Mahundi

Agizo hilo amelitoa mara baada ya kukuta mradi unaendeshwa na pampu moja ambayo inazidiwa nguvu kutokana na wingi wa maji katika chanzo hicho kinachotokana na maji ya Ziwa Victoria.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa maji safi na usafi wa mazingira mjini Geita, Mhandisi Frank Changawa, amesema mradi huo walikabidhiwa Januari mwaka huu na kufikia mwezi Machi utakuwa umekamilika.