Ijumaa , 17th Feb , 2017

Oparesheni za kuwakamata watuhumiwa wanaojihusisha na dawa za kulevya nchini imefanikiwa kukamata watuhumiwa wawili waliohusika kupitisha kemikali bashirifu za dawa hizo aina ya ephedrine huku wengine wawili wakiwa bado wanasakwa na polisi

Kamishna wa Oparesheni wa Mamlaka, Mihayo Msikhela akizungumza na wanahabari

Akitoa taarifa hiyo leo Jijini Dar es Salaam Kamishna wa Oparesheni wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Bw. Mihayo Msikhela amesema watuhumiwa hao ni wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na wamegundulika baada ya kufanya uchunguzi wa ripoti ya majina iliyokabidhiwa kwao na uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam.

Kamishan Msikhela amesema taratibu zinazotumika kwa sasa za kuwakamata watuhumiwa wa madawa ya kulevya ni za kiusalama zaidi ili kuzuia watuhumiwa wasipoteze ushahidi.

Aidha, Kamishna Msikhela amesema katika operesheni ya kupambana na dawa za kulevya inayoendelea nchini mikoa ya Simiyu, Mara na Lindi inaongoza katika uteketezaji wa madawa ya kulevya ya bangi na mirungi kwa kipindi cha siku nne.

Msikilize hapa Kamishna Misikhela