Jumapili , 27th Sep , 2020

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu amewataka Watanzania kuwa na utaratibu wa kupima afya zao mara kwa mara kwa kuwa taifa lenye watu wenye afya njema ni mtaji wa kwanza kwa nchi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu.

Mhe. Zungu ametoa wito huo mara baada kufanya mazoezi ya pamoja katika viwanja vya Tanganyika Packers Jijini Dar es Salaam yaliyoandaliwa na Hospitali ya Aga Khan yaliyoendana na upimaji wa magonjwa mbalimbali bila gharama,  yakiwemo ya saratani ya matiti kwa wakina mama, ambapo amekumbusha umuhimu wananchi kulinda afya zao.

"Mhe Rais anataka Taifa la watu wenye afya njema hivyo ukiona watu wanajitokeza hivi kuandaa maeneo watu waje kupima afya bure ni jambo kubwa sana niwaase tuu watanzania wote kuitumia fursa hii",amesema Zungu.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye zoezi hilo wameshauri kutolewa mara kwa mara kwa huduma za upimaji afya bure kwa wananchi kwa kuwa wengi wao huwa wanashindwa kumudu gharama za vipimo.