Ijumaa , 15th Oct , 2021

Wanawake wa Kata ya Mtama, Halmashauri ya Mtama mkoani Lindi, wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya katika kata yao, ambazo ni sehemu ya mapato ya tozo za miamala.

Simu

Wakizungumza na EATV  wanawake hao wamesema kuwa ujenzi wa kituo hiko cha Afya utaenda kupanua huduma za uzazi pamoja na huduma zingine walizokuwa wakizipata kutoka katika zahanati pamoja na kupunguza gharama ya kusafiri kwenda Hospital ya Nyangao kwa ajili ya kupata huduma hizo huku wanaume nao wakigongea msumari changamoto wanazokabiliana nazo wake zao pindi wanapokuwa wajawazito.

Hayo yote yamejiri hii leo Oktoba 15 ikiwa Mataifa yote ulimwenguni yanaadhimisha Siku Wanawake Vijijini.