Jumapili , 15th Jan , 2017

Wakazi wa wilayani Pangani mkoani Tanga waliokuwa wakiishi kwa kutegemea zao la nazi, huenda wakakumbwa na hali mbaya ya maisha ikiwemo njaa kutokana na zao hilo kuyumba wilayani humo.

Jumaa Aweso akiwa kwenye kipindi cha Weekend Breakfast , cha EA Radio

Mbunge wa jimbo la Pangani, Jumaa Aweso akiwa kwenye kipindi cha Weekend Breakfast cha Jumapili, kupitia East Africa Radio, amesema hali ya uzalishaji wa zao hilo kwa sasa ni mbaya, na hivyo kuitaka serikali kufanya utafiti kujua chanzo cha hali hiyo.

Amesema sehemu kubwa ya wakazi wa Pangani wanaishi kwa kutegemea zao hilo, hivyo ni vyema jitihada za haraka zikafanyika, huku akishauri kuwekwa utaratibu mbadala wa kilimo cha umwagiliaji kwa ajili ya mazao mengine wakati ambapo nazi imeshuka.

Msikilize hapa Jumaa Aweso akizungumza na EATV kuhusu suala hilo-