Alhamisi , 22nd Jun , 2017

Mawakala wa Ajira na Watanzania wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi hususani nchini za kiarabu wametakiwa kupitia kwenye mfumo uliaondaliwa na serikali ili kuepusha unyanyasi, ukatili ukiwemo mauaji yanayowakuta katika nchi wanazokwenda kufanya kazi

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde na kusema lengo likiwa ni serikali kupata taarifa pindi manyanyaso dhidi yao yanapojitokeza.

Mhe. Mavunde ametumia fursa hiyo kutoa onyo kwa Mawakala ambao husafirisha watu kinyume na taratibu na kusema kuwa pindi watakapobainika sheria kali zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo kufutiwa usajili, na kuwachukulia hatua ya kutopata usajili tena na kuongeza kwamba wapo watanzania hawapiti katika ofisi za serikali  kitu ambacho kinawafanya wakose hata msaada wa haraka kutoka ubalozini.