Ijumaa , 17th Feb , 2017

Waziri wa Sheria na Katiba Dkt. Harrison Mwakyembe amesema licha ya sheria kuweka adhabu ya kifungo kwa watu wanaotumia dawa za kulevya, bado kuna nafasi ya watu wa aina hiyo kusamehewa endapo watajitokeza mapema, kukiri na kuahidi kuacha.

Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe

Dkt. Mwakyembe amesema hayo wakati akitoa elimu juu ya sheria mpya ya kupambana na kudhibiti dawa za kulevya, kupitia kipindi cha East Africa Breakfast cha EA Radio, na kutolea mfano baadhi ya wasanii ambao walitajwa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, ambao baadha ya kuhojiwa walikiri kutumia na kuahidi kuacha.

Amesema kama mtu anatumia, halafu akawa anakataa kiasi cha kulazimu uchunguzi hadi kufikishwa mahakamani, huyo atapelekwa mbele ya sheria ichukue mkondo wake.

Msanii TID alipowaomba radhi watanzania na kutangaza kuacha matumizi ya dawa za kulevya

Baadhi ya wasanii ambao walikiri kutumia dawa hizo, na kuwekwa chini ya uangalizi wa mahakama kwa mwaka mmoja na wengine miaka miwili ni pamoja na TID, Tunda, Petit Man na wengine.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, sheria imetoa adhabu kwa mtumiaji wa dawa hizo kufungwa gerezani miaka mitatu.

Huyu hapa Dkt. Mwakyembe